Sunday, July 24, 2011

LOVENESS FLAVIAN AVIKWA TAJI


Hatimaye kitendawili cha nani ataibuka Vodacom Miss kanda ya Mashariki 2011 kimetenguliwa na jo
po la majaji limemtangaza Miss Lindi 2011, Loveness Flavian (20) na Msomi wa Chuo Kikuu cha Makere al
iye na Shahada ya Mahusiano ya Kimataifa kuwa ndie mshindi.

Loveness ambaye alionesha mapema kuwa kinara wa washiriki wengine 10 licha ya kuvalia namba 10 sasa ataungana na warembo Asha Salehe na Mariaclara Mathayo kuingia katika kambi ya Miss Tanzania 2011 kutoka Kanda ya Mashariki.
Vodacom Miss Eastern Zone 2011, Loveness Flavian (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Asha Saleh (kushoto) na Mariaclara Mathayo aliyeshika nafasi ya tatu.
Loveness alipotajwa kuwa ndie mshinde alilia kwa furaha na hakuamini alicho kisikia.
Miss Eastern Zone Flora Florence aliyemaliza muda wake akimvisha taji Loveness Flavian.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya 5 bora ya Miss Kanda ya Mashariki. Kutoka Kulia ni
Ritha Kavishe, Rahma Swai, Mariaclara Mathayo, Loveness Flavian na Asha Saleh
Hawa ni washiriki wote wa Miss Kanda ya Mashariki

No comments:

Post a Comment