Thursday, July 28, 2011

LUDACRIS AWASILI BONGO


Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni hii ndani ya Kempinsk hotel na Clouds TV,mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,litakalofanyika jumamosi hii ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onesho lake moja ndani ya viwanja vya Lidaz Club jijini Dar.
Ludacris akijiweka sawa kwa ajili ya kurekodiwa na Wana Wa Clouds TV jioni ya leo.
Muwakilishi kutoka Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akiwafafanulia jambo Wageni aliokuja nao Mwanamuziki Ludacris jioni ya leo akitokea nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment